.
HABARI YA MLIPUKO-ARUSHA CHANZO KINASEMA, BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA
TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO.
CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUNA GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO
BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA
HIZI NI BAADHI YA PICHA KATIKA ENEO HUSIKA:
waathirika wa mlipuko huo
.
kanisa ambapo mlipuko umetokea
..
Waumini pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki wasiamini nini kilichotokea kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea asubuhi ya leo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo. JESHI la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia mtu mmoja ambaye anahusishwa na kutokea kwa mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki la St Joseph Olasiti Arusha leo asubuhi. Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Papa kutoka Vatican akizindua Parokia hiyo mpya ya St Joseph Olasiti ya Jijini Arusha. |
Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia. |
No comments:
Post a Comment