Wednesday, February 20, 2013

KUNA NINI KATI YA DIAMOND PLATNUMZ NA TANZANITE?

...http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/02/tanzanite_diamond.jpg

 ..Tanzanite

sasa hii inaleta picha ya kutoeleweka kuwa kuna nini kinaendelea kati ya diamond na msanii mwenzake tanzanite..hili linatokana na wasanii hawa kutokuwa na hali ya kuelewana kati yao kwa miaka kadhaa sasa.

Hali hii inatokana na Tanzanite kibuka na kumshtumu Diamond kuwa amemuibia wimbo wake wa ''MBAGALA'' pale alposema kuwa ni wakwake, hili lilileta mtafaruku kati yao na baada ya muda mambo yakatulia.
 baadaye akachukua beat ya wimbo wa ''NITAREJEA'' wa diamond na kurekodi bila ruhusa ya diamond
http://3.bp.blogspot.com/-Mko4hfzwJlg/ULnYMjhQO8I/AAAAAAAARp0/1kqpj2rKxYM/s1600/tanzanite.bmp
Baada ya kipindi fulani tanzanite akaibuka na kusema kuwa diamond kamloga na anaumwa magonjwa ya ajbu na ameenda kwa mganga na kuambiwa kuwa diamond amemloga
akajitokeza katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini na kutangaza swala hilo na kumuomba diamond amsamehe kwa hilo.
 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/02/2c9a5e42790e11e2b9fd22000a1fbc16_7.jpg
 Katika hali ya kushangaza msanii huyu tena ametoa wimbo ambao anadai ameshirikishwa na diamond,
DIAMOND amekana kuhusu kumshirikisha huyu jamaa katika huo wimbo na kuwa wimbo huo bado hajautoa na ulikuwa bado haujamalizika na huyu TANZANITE ameiba na kwenda kurekodi na kuweka sauti yake na kuuusambaza kana kwamba amefanya kolabo na diamond.
Diamond akiongea na moja ya vituo vya redio  leo hii amelaani hali hii na kusema hajui huyu Tanzanite anataka nini .



No comments: