Tuesday, May 07, 2013

CHIDI BENZI ASHUHIWA KIPIGO NA KALAPINA NDANI YA MAISHA CLUB {TAZAMA VIDEO HII}

msanii wa hip hop bongo chidi benz amejikuta matatani kwa kuchezea kichapo kutoka kwa msanii mwenzake KALAPINA pale alipoingilia shoo yake maisha club
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhFpvDtT46-roDa_WcRYYUPBLQtsc51v3VFNddONCrp1ad5Mg-rxeIIY-uAQLpuV9Zv6REhjGcAPEP2vQJwAGyEHk170U7onXcwkoliMbzuvLA-tOY8PJB88kLLPCmr8Jkz4Zneed7jGcQ/s1600/pina+&+chidi.jpg.

 http://4.bp.blogspot.com/-i9sJKitCytY/UYkZodR7bgI/AAAAAAAAffA/N5aWVqEakKg/s1600/KICHAPO.jpg.

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg10XoWYiYgAinyirXKSW9DtewRTFz0stEEu7e8QRhKVkJmZcm03UuaXXier9UgpxIs5uK-grIhnDz8NG_GIjXGFEPg29fhfzLbOaFLwOclXmXGlrWxT1VX6RWkDn-vAAV9gbWEmiYytoM/s1600/IMG_3814.JPG
TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA HAPA

HII NDIYO INTERVIEW YA MKURUGENZI WA CLOUDS FM, RUGE MUTAHABA KUHUSU TUHUMA ZA JAYDEE

Hiki ndicho alichoongea mkurugenzi wa clouds FM Ruge Mutahaba akitolea ufafanuzi kuhusu tuhuma alizotoa lady jaydee!!!
Sikiliza interview hapa
ruge-mutahaba-lady-jaydee-clouds-fm

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA LADY JAY DEE KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK BAADA YA INTERVIEW YA RUGE

Sakata la Lady JayDee na wakurugenzi wa Clouds FM, Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga, halionyeshi dalili za kupungua kasi muda wowote hivi karibuni. Baada ya Ruge kuzungumzia kwa kirefu drama hiyo kwenye interview.Jide ameendeleza harakati zake dhidi ya mapedejhee hao kupitia Twitter na Facebook, ambapo alianza kwa kuwapa washabiki wake teaser ifuatayo 

at Facebook: “Kama mtakumbuka niliahidi kutoa awamu ya pili tar 15 au 17 May na ahadi ni deni..Japo naona mbali ila Nitafanya hivyo, bado nina mengi sana ya kuzungumza kuhusu Ruge na wenzake…Ile ilikuwa ni trailer tu, Movie ndio linaanza sasa #TeamAnaconda no surrender”


 lady-jay-dee-ruge-mutahaba-clouds-fm-twitter-interview-0

Sunday, May 05, 2013

CHANZO CHA MLIPUKO ULIOTOKEA KANISANI ARUSHA HIKI HAPA {PICHA ZA TUKIO}


.
HABARI YA MLIPUKO-ARUSHA CHANZO KINASEMA, BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI WAUMINI WA KANISA HILO LA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA
TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO.
 
CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUNA GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO
 
BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA
 
HIZI NI BAADHI YA PICHA KATIKA ENEO HUSIKA:
 
..
 waathirika wa mlipuko huo
.
kanisa ambapo mlipuko umetokea


..
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjv8SsgP_YYAu0fkttwumLERJZKYfR18BuBmZi1wfHtWFYk3vObIobK_PFKULGI4dw-thebGDHsmJQKys-krh_8XxMpPdM84SuV3g9teCjKStVWb1f1kRF1Hszm9exO3-M3oWxrgGNew1Hi/s1600/IMG_20130505_130432_0.jpg Waumini pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki wasiamini nini kilichotokea kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea asubuhi ya leo.
 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ibrahim Kilongo.


JESHI la Polisi Mkoani Arusha linamshikilia mtu mmoja ambaye anahusishwa na kutokea kwa mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki la St Joseph Olasiti Arusha leo asubuhi.

Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Papa kutoka Vatican akizindua Parokia hiyo mpya ya St Joseph Olasiti ya Jijini Arusha.
Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia.

 

Saturday, May 04, 2013

NEW SONG; VISIOR CMB FT WIZ KENNETH "WAKASEMA" DOWNLOAD AND LISTEN FROM HERE

hii ni new song iliyofanywa na VISIOR CMB ambaye ni mmliki wa blog hii akimshirikisha WIZ KENNETH ni ujio mpya!!! wimbo umefanywa STIM RECORDS chini ya producer stim master!!

na huyu ndiye visiorCMB



visior CMB alipokuwa akirekodi wimbo huu
DOWNLOAD AND LISTEN THIS SONG FROM HERE

PADRI ALIYENASWA NA MKE WA MTU " MUME AIBUKA NA KULIPONDA KANISA KATOLIKI"

LILE saga la madai ya fumanizi la Padri Urbanus Ngowi aliyekuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishiwa Makomu, Marangu limeibua mtikisiko mkubwa kwa Kanisa Katoliki nchini, .
 


Katika habari iliyofichuliwa , Aprili 29 hadi Mei 5, mwaka huu, ilidaiwa kuwa Father Ngowi alinaswa chumbani akiwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina la kijamii la Mama P. Mara baada ya ‘mzigo’ huo kuingia mitaani nchi nzima, mhariri wa gazeti hilo (jina linahifadhiwa) alianza kupokea simu na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka kona mbalimbali kwa watu waliojitambulisha kuwa ni waumini wa kanisa hilo wakidai kushtushwa na tukio hilo.  

Habari za ndani kutoka Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi zilieleza kuwa baada ya ishu kuwa ‘hoti’, viongozi wa jimboni hapo, Jumatatu iliyopita walikaa vikao vizito kulijadili suala hilo na kulitolea uamuzi. Ilidaiwa kuwa uongozi ulikubaliana kumwita mume wa Mama P ambaye wakati tukio hilo likitokea alikuwa jijini Dar es Salaam kwa shughuli zake binafsi. Ilisemekana kuwa waliwasiliana na mwanaume huyo ambaye alitakiwa kuondoka Dar, Alhamisi iliyopita kwenda Moshi kukutana na viongozi hao kwa lengo la kuweka mambo sawa. Ilidaiwa kuwa jamaa huyo ambaye amezaa na Mama P watoto wawili, alikubali kukutana na viongozi hao kwa shingo upande huku akitishia kulipeleka suala hilo mbele zaidi kwa kuwa alishalalamika muda mrefu kwamba Father Ngowi ana ukaribu wenye maswali mengi na mkewe.

Tulitonywa kuwa baada ya mwenye mke huyo kulalama sana, Father Ngowi aliitwa na uongozi wa jimbo hilo kisha akaonywa lakini hakuna kilichobadilika. AHADI NI DENI Ili kujua uamuzi uliofikiwa ambao Mwakilishi wa Mkuu wa Jimbo la Moshi, Father Paul Uria alimuahidi Mhariri wa Ijumaa Wikienda kuwa Jumatatu iliyopita saa 10:00 angemweleza, alipigiwa simu ambapo mambo yalikuwa hivi: Mhariri: Pole na majukumu Father Uria. Father Uria: Nashukuru, nazungumza na nani? Mhariri: Mimi ni yule mhariri (akitajiwa jina) ambaye tulizungumza Ijumaa iliyopita juu ya lile tatizo la Father Ngowi. Father Uria: Naam, unasemaje? Mhariri: Uliniahidi nikupigie simu leo muda huu ili uniambie jimbo limefikia uamuzi gani juu ya suala hilo baada ya kukaa kikao. Father Uria: Nipo njiani naendesha gari (akakata simu). Saa moja baadaye, Father Uria alipigiwa tena simu lakini iliita bila kupokelewa. UJUMBE MFUPI Baadaye alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kupitia simu yake ya kiganjani lakini hakujibu. Mambo yalipogonga mwamba kwa Father Uria, alipigiwa Father Ngowi ili kujua mustakabali wake juu ya sakata hilo, akawa anakata simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi naye hakujibu. JUMANNE WIKI HII Kesho yake (Jumanne iliyopita), Father Uria alipigiwa simu kwa namba tofauti, alipopokea na kusikia utambulisho alikata simu na alipopigiwa mara nyingine hakupokea. Kwa upande wake, Father Ngowi naye alipokea bila kusema chochote, akasikilizia anayepiga na aliposikia utambulisho alikata simu. MUME WA MAMA P ASAKWA Tulimsaka kwa udi na uvumba mume wa Mama P (Mama Peter), Bw. Pasian Mallamsha ambapo Jumatano iliyopita alijaa kwenye kumi na nane na kueleza ya moyoni mwake kuhusu tukio la mkewe na Father Ngowi. Kwanza mwanaume huyo alikiri kwa njia ya simu kuwa, Mama P ni mkewe na ‘P’ ni herufi ya kwanza ya jina la mmoja wa watoto wao aitwaye Peter.

 “Kwanza nashukuru kwa kunipigia. Nimesikia kilichotokea na ni kweli nimeitwa jimboni Moshi kwa hiyo naelekea huko kusikia walichoniitia. “Kilichotokea kimedhihirisha malalamiko yangu ya muda mrefu juu ya Father Ngowi niliyokuwa nikiyapeleka pale jimboni. Ngoja nikawasikilize lakini lazima kieleweke,” alisema mwanaume huyo. Tulimuomba Baba Peter kukutana naye uso kwa uso kwa ajili ya mahojiano zaidi lakini ilishindikana kwa kuwa alitaka kupata ushauri kwanza kutoka kwa kaka yake hivyo bado anasubiriwa kufunguka zaidi.

Wakizungumza juu ya sakata hilo, baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki mjini Moshi, walimuomba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo kulitolea tamko suala hilo ili kutuliza upepo na kumaliza ‘sintofahamu’ ya mustakabali wa Father Ngowi. “Jambo hili ni zito na linalitia aibu kanisa na waumini wake. Tunaomba Kadinali Pengo atoe sauti ili tujue msimamo wa kanisa,” alisema Paulo Swai, mkazi wa mjini Moshi. Hivi karibuni, Father Ngowi alikutwa na mkasa wa kudaiwa kufumaniwa akiwa kwenye nyumba yake paroki

Wednesday, May 01, 2013

WOSIA ALIOTOA LADY JAY DEE "AWATAJA WABAYA WAKE NA KUSEMA WASIHUDHURIE MAZISHI YAKE"

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/03/578551_10151281152335025_1668082456_n.jpg.
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOYxfVN5XzfBcd0LNThrGKJOW6Ns-stbhhZxDaow6U1JPoG5hrRmYQThSi3_Yys00EwNLpwlPWnSNNueSxVqapwMKmdFfmUjNy87UqGM-SY4TbTw9iXMc_74BMXAuArh84ZHOdPQkRtOKT/s1600/lady_jay_dee.jpg
 
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.

Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

Tuesday, April 23, 2013

THE WORLD OF WONDERS "UPSIDE DOWN HOUSES" AU "NYUMBA ZILIZOJENGWA JUUCHINI"

hizi ni picha ya nyumba ambazo zimejengwa kwa muonekano tofauti kwamba zinatazama chini kwa maana muonekano wake ni kama paa la nyumba lipo chini
TAZAMA NYUMBA HIZI UJIONEE MWENYEWE

http://cdn.freshome.com/wp-content/uploads/2007/09/upside-down-house2.jpg.

 http://blog.petaflop.de/wp-content/uploads/2007/12/wonderworks-upside-down-house-haus-auf-dem-kopf-smoky-mountains-pigeon-forge-tennessee-tn-usa.jpg.

 http://i.telegraph.co.uk/multimedia/archive/00801/upside-down-house_801556i.jpg.
\
 http://resources0.news.com.au/images/2010/03/16/1225841/270284-upside-down-house.jpg.
 huu ndo muonekano wa ndani

 http://farm5.staticflickr.com/4078/4778823567_62d3c7a4aa_z.jpg.

 http://www.ripleys.com/weird/files/2012/05/UpsideDownHouse5.jpg.

 http://cdn0.lostateminor.com/wp-content/uploads/2012/05/UpsideDownHome2.jpg.

 http://1.bp.blogspot.com/-RnT9gr1Xs_k/T7e1-huU22I/AAAAAAAAKDQ/dL0cmt70euI/s1600/upside-down-house-sabah.JPG

Saturday, April 20, 2013

LIL WAYNE "TUNECHI" IN TROUBLE

http://assets.nydailynews.com/polopoly_fs/1.172064.1314040956!/img/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/landscape_635/alg-court-lilwayne-jpg.jpg It has been reported that legendary producer, Quincy Jones and his lawyers have filed papers to have Lil Wayne’s multi-million dollar mansion and Bugatti Veyron car seized in order to settle a lawsuit again the rapper.

Quincy Jones filed a counter-suit against Lil Wayne for US$3.4 million after Lil Wayne himself filed a lawsuit against Jones. Weezy’s lawsuit stemmed from a documentary about the rapper that chronicled his addiction to Codeine. The rapper then made an effort to quiet the documentary’s release. Jones’ suit is against Lil Wayne for sabotaging the marketing of the documentary.

Lil Wayne’s camp however denies these claims and states that Lil Wayne will have no issues settling the matter before his property and assets are seized.

MAKAHABA WAWAVALIA NJUGA POLISI

http://1.bp.blogspot.com/--rWzm9iVdsE/UIc-gPL6IMI/AAAAAAAABT0/uW-W06MAnKU/s1600/MALAYA+WA+DAR.jpg
Jeshi la Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, limelalamikiwa kwa vitendo vya baadhi ya askari wake kuvamia vyumba vinavyodaiwa kupangwa na watu wanaodaiwa kuwa makahaba (madanguro) na kuwapora fedha, simu na vitu vingine vya thamani nyakati za usiku.

Aidha, askari hao wamedaiwa kuwageuza wanawake hao mashine za kutolea fedha (Atm) ambapo hufika katika vyumba vyao kila baada ya wiki moja na kuwadai fedha kati ya Sh.30,000 na 50,000 kila mmoja kama hongo ili wasiwafikishe polisi.

Malalamiko hayo yametolewa na baadhi ya akina mama wanaoishi eneo la Mwananyamala walipozungumza na NIPASHE baada ya askari hao kukamata wanawake zaidi ya 87.
Kiongozi wa wanawake hao, Judith Rugamwa alidai kuwa, askari hao kutoka vituo vya Oysterbay na Mabatini wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga, jambo ambalo ni kinyume cha haki zao binadamu.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZYTxnUCJG-rae7vhZYLv1sVQFY-yg1aHPlIWVhq7KUhqX8XvJ62bW8qFZAVkKHx2sQOz7NeU4DO4W-G30u2JMLcWcrDqVoP-4l-TN3n5CteAFfJP8uFylCxZIJ-gQixdim__JPk0qye8/s1600/African.jpg
"Wakitukamata huwa wanasema kosa letu ni kufanya ukahaba, lakini tukifikishwa kortini kosa linabadilika na kuwa uzembe na uzururaji, wakati wametukamata vyumbani kwetu ," alisema Judith.

Alisema wamechoka kunyanyaswa kama wakimbizi na kuonya kuwa sasa wanajiandaa kupambana na kila askari atakayefika hasa nyakati za usiku na kuwavunjia milango ya vyumba vyao ili kuwamata na kuwalazimisha wawape fedha huku wakimtaja afande Swai na Emma kuwa ndiyo wanaoongoza uovu huo.
Akizungumzia tuhuma hizo, afande Swai alijitetea kuwa yeye binafsi hajawahi kushiriki katika kuomba fedha wala kupora simu za wanawake hao licha ya kukiri kuwa ndiye anayeongoza misako yote Kinondoni.

"Kuhusu madai ya kuomba fedha, siwezi kukataa kwa sababu mimi huwa siingii vyumbani kukamata wanawake hao, badala yake askari wangu ndiyo wanaohusika moja kwa moja kabla ya kuwaleta katika gari ambayo huwa nawasubiri, lakini kama wanafanyiwa hivyo naomba wawataje kwa majina askari hao," alisema.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhiAkn3MGj30zEYS5SeEWETKg4jrTyz4-WRCGQL0MA1Zb5cS1guySfjeQqAXv9tZUsw8UpLvceGABG7-w8x_vrXMk33ykcZhugxOQMz8srkmbBtpH0y3hdo2Oo2Prl49TmQA31D4ou2X3ob/s1600/MALAYA.jpg
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani wa Kinondoni (RPC), Charles Kenyela, alisema amri ya kuwasaka na kuwakamata makahaba hao huwa inatolewa na ofisi yake na kwamba madai ya polisi wake kuchukua fedha na simu za watuhumiwa ni uongo mkubwa.
"Kama kuna mtu amewahi kufanyiwa hivyo aje ofisi kwangu na ushahidi ili ofisi yangu ichukue hatua kali za kinidhamu kwa sababu anayeshawishi, anayetoa na kupokea rushwa wote wanafanya makosa, waache kulalamika waje niwasilikize," alisema Kenyela.

MAUAJI DAR, "MTU MMOJA AUAWA KIKATILI"


 kamanda wa polisi,mkoa wa kipolisi temeke engelbert kiondo

Mtu mmoja jijini Dar es Salaam ameuawa kinyama kwa kupigwa, kisha mwili wake kuingizwa ndani kiroba na kutupwa ndani ya mtaro wa maji. Mwili wa mtu huyo umeokotwa jana majira ya saa 2:00 asubuhi eneo la Nyamachoma Yombo Buza baada ya wakazi wa eneo hilo kusikia harufu kali kutoka kwenye mtaro wa maji machafu pembeni ya barabara ya Yombo.

Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo, walisema mwili huo wa mtu mwanaume ulikutwa ukiwa umewekwa ndani ya viroba viwili, kisha kutupwa kwenye mtaro kama takataka na watu wasiojulikana. Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina mama Hassani, alisema chanzo cha kugundulika ni harufu kali iliyokuwa ikitoka kwenye mfuko huo na kusambaa eneo lote. "Baada ya kusikia harufu, tulianza kusaka inatokea wapi, ndipo tulipogundua inatoka kwenye mzigo wa kiroba uliokuwa ndani ya mtaro wa maji," alisema mwanamke huyo.

 Alisema, kutokana na hali ya mzigo huo, walijua ndani yake kuna takataka, lakini walipoondoa kiroba hicho walikuta miguu ya mtu. Hata hivyo, walishindwa kuendelea kuondoa kiroba kingine na kuamua kuwaita polisi ili kwenda kuuchukua mwili huo. "Inaelekea mtu yule aliuawa siku tatu zilizopita nyakati za usiku, kwa sababu ndani ya kiroba alikuwa katika hali ya kuchuchumaa na mikono yake imefungwa kamba kwa nyuma," alisema mkazi mwingine Abubakar Saidi. Mashuhuda hao walisema askari polisi walifika eneo la tukio majira ya saa 4:30 asubuhi na kuuchukua mwili huo na kuupeleka kituo cha polisi Chang'ombe. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema bado hajapata taarifa kuwepo kwa tukio hilo.