Breaking
News: Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam
Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa jana kuamkia
leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam mara tu
baada ya kujifungua .
Mariam Khamis umauti umemkumba akiwa
anaimba kundi la TOT plus lakini enzi za uhai wake aliwahi kuimbia
katika makundi mbalimbali ya taarab likiwemo East Africa Melody,
Zanzibar Stars na 5 Stars.
Khamis Muhidini Shomary baba wa
marehemu amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo
anatarajiwa kuzikwa hapo kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment