Friday, November 23, 2012

SUGU NA FID Q SASA KATIKA MOVIE

Wasanii mahiri wa Bongo Fleva wanaokubali katika tasnia hii ya muziki hapa Tzee kwa kazi zao nzuri za muziki wanazojihusisha nazo,sasa latest info ni kwamba kampuni inayofahamika kwa jina la Papaz Arts & Promoters Entertainment chini ya msemaji bwana Issa Kipemba alisema japokuwa wao kampuni wamekuwa wakisaidia na kusamba kazi za wasanii wa hapa Tzee sasa wameamua kusambaza filamu zao na kuwaunganisha wadau wengine katika tasnia ya filamu ,ndio maana unaona katika filamu hii mpya ya Bifu, Mh. Mbilinyi naye ameamua kushirikia katika harakati za kuipa nguvu tasnia ya filamu.Kwa mujibu wa Issa Kipemba alisema kwamba Filamu ya Bifu inawashirikisha wasanii kama  Fid Q, Sugu, wakiwa sambamba na wasanii wengine lengo likiwa ni kujaribu kuonyesha hisia zao kwa kupitia tasnia ya filamu baada ya kuimba sana katika muziki na kuhisi kama hisia zao kukosa msikilizaji,  filamu ya Bifu itaeleza maisha halisi ya wasanii wa Bongo maarufu kama Bongo Fleva.

No comments: