Wednesday, January 30, 2013

DIAMOND PLATNUMZ ASEMA ''AMEAGA KWAO''

Ni baada ya maneno ya hapa na pale kutoka kwa watu mbalimbali wakisema kwamba diamond ameshuka thamani na hana ustaa kama alivyokuwa mwaka 2012. Ni kwamba eti  Diamond amechuja na kapoteza ile heshima ya ustaa aliyokuwa nayo hapo mwanzoni.

Hii imekuja baada ya Profesa Jay kutweet kuhusiana na suala hili  na pia habari katika magazeti kuhusu  kuporomoka kwa ustaa wa Diamond.Lakini Diamond mwenyewe amekanusha habari hizi na kusema kuwa si za kweli na hakuna kitu kama hicho

Akihojiwa na millard ayo diamind amesema yeye bado ni staa na hajapoteza ustaa wake kwani yeye ndiye msanii pekee anayelipwa pesa nyingi ama mkwanja mrefu kabisa katika shoo zake  na pia hakuna msanii yoyote kibongobongo anayeweza kufanya shoo na kujaza watu wengi zaidi kama yeyena akasema yeye ameaga kwao na hakuna atakayeweza kumshusha kwa kumzushia mambo yasiyo ya kweli

yote kwa yote ukweli utabaki palepale kuwa diamond ndo msanii aliyeng'ara zaidi mwaka 2012

No comments: