Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo, aliiambia NIPASHE
katika mahojiano jana kuwa taratibu zote kwa ajili ya kutangaza matokeo
hayo zimekwisha kukamilika na sasa yatatangazwa rasmi leo.
Wiki iliyopita Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa,
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza ajira mpya za
walimu aliahidi kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yatangazwa
mwishoni mwa wiki hiyo, lakini hata hivyo hayakutangazwa.
Dk. Kawambwa ambaye aliulizwa ni kwa nini matokeo ya mtihani huo
yanacheleweshwa kutangazwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, alisema
kimsingi hayajachelewa kwa sababu wanafunzi watakaochaguliwa kuingia
kidato cha tano wanatakiwa kuripoti mwezi Julai mwaka huu.
No comments:
Post a Comment