Uongozi wa lebo ya Cash Money
yenye miliki ya vichwa kibao wakiwemo Nicki Minaj, Lil Wyne, Drake,
Tyga, Busta na wengine.. umesema kuna upotoshwaji mkubwa juu ya taarifa
za kuzidiwa kwa Lil Wyne ambae amelazwa hospitali toka wiki iliyopita
huku media mbalimbali zikiripoti rapper huyo kuwa kwenye hali mbaya sana
kiafya ambapo kalazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Hata hivyo uongozi wa Cash
Money umethibitisha kwamba mshkaji yuko salama na afya yake ni nzuri
sasa hivi ndio maana imani yao ni kwamba atatoka hospitali very soon na
kusisitiza kwamba taarifa za Wyne kuwa mahututi zilizosambaa mwanzoni
zilikua za uongo.
Chanzo cha habari kilichokua
kinatoa info kwa TMZ kimesema muda mfupi uliopita Lil Wyne ameonekana
mwenye nafuu na hata kuweza kutembea humohumo ndani ya hospitali akiwa
na walinzi wake.
No comments:
Post a Comment