Kassu Ent iliandaa tamasha maalum kutoka kwa wasanii wetu wa kizazi kipya iliowajumuisha Barbaba na Suma Lee. Tamasha hili lilikwenda sambamba kwa kusherekea miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika siku ya jumamosi tarehe 22.12.12 jijini London katika ukumbi wa Stratford.
Mgeni rasmi alikua naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na mkewe Irene Kilumanga. Aidha Mh Balozi Kilumanga aliwapongeza watanzania walioweza kuja kujumuika na kusherekea pamoja katika siku hii na kuwasihi kuendeleza mshikamano kwa kuishi pamoja kwa amani na upendo.
No comments:
Post a Comment