Monday, December 31, 2012

VANESSA MDEE KUTAMBULISHA NGOMA YAKE MWAKANI

Baada ya kufanya vizuri katika collabo mbili kati ya A.Y na Ommy Dimpoz aliweza kufahamika  na kupelekea mashabiki wengi kumkubali katika muziki wa Bongo Fleva,Sasa kama unakumbuka siku ziliyopita alifunguka katika ukurasa wake wa twitter na akasema kwamba anatarajia kuachia ngoma yake mpya siku ya tarehe 26 mwezi huu lakini mpaka sasa kimya ni tatizo.
 Leo kupitia Double XXL aliamua kufunguka na kusema kwamba amekuwa na mambo mengi sana na ndiyo maana hakuweza kuitambulisha katika vituo mbalimbali vya ma radio ila anatarajia rasmi kuiachia mwakani mwezi wa kwanza tarehe 12.Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa Vanessa Mdee kaa tayari kwa ujio mpya kutoka kwake.

No comments: