Friday, February 08, 2013

ASKOFU LASER AFARIKI DUNIA



 Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini na Kati, Thomas Laizer, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Israel Karyongi, Askofu Laizer, alifariki dunia jana saa 12: 00 jioni.

Askofu Laizer alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha, kwa zaidi ya miezi miwili. Hata hivyo, haikufahamika marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa gani.
Juzi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimtembelea katika hospitali hiyo inayomilikiwa na KKKT kumjulia hali.

Awali, Askofu Laizer alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, mkoani Kilimanjaro.

No comments: