Hatimaye Goldie aliyefariki dunia siku kumi nambili zilzopita amezkwa jana huko lagos nchini Nigeria.
msiba wake huo umefanyika kwa siri na baadhi ya watu walialikwa kwa mazishi hayo
na hizi ndo picha za mazishi ya GOLDIE HARVEY!!
PICHA ZA MAZISHI YA GOLDIE HARVEY
...
picture with millardayo.com/
Tuesday, February 26, 2013
Monday, February 25, 2013
DALADALA YAUA WAWILI DAR NA KUJERUHI 46
Abiria wawili wamefariki dunia na wengine 46 kujeruhiwa katika ajali
mbili zilizohusisha magari manne, zikiwamo daladala tatu walizokuwa
wamepanda na Fuso, kugongana katika maeneo tofauti, Wilaya ya Temeke,
jijini Dar es Salaam.
Kati ya waliofariki, mmoja ametambuliwa kwa jina la Sabrina Is-haka
(11), ambaye alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali
ya Wilaya ya Temeke.
Mwingine mwanaume, ambaye jina lake halijafahamika, anayekadiriwa
kuwa na umri wa kati ya miaka 30-31, alifariki dunia papo hapo katika
eneo la ajali.
Mkuu wa askari polisi wa Kikosi cha Usalama wa Barabarani Mkoa wa
Temeke, Prackson Rugazia, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Pia Mwangalizi Mkuu wa jana wa Hospitali hiyo, Amosi Kaberege,
alithibitisha hospitali yake kupokea majeruhi hao pamoja na miili ya
watu waliofariki kuhifadhiwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa Kaberege, marehemu Sabrina, ambaye alikuwa na pacha
mwenzake katika gari lililopata ajali, alifariki dunia kutokana na
kutokwa na damu nyingi baada ya kukatika mguu.
Aidha, kati ya waliojeruhiwa, 42, akiwamo pacha wa marehemu Sabrina, walitibiwa katika hospitali hiyo na kuruhusiwa.
Hata hivyo, majeruhi wawili kati yao, walihamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa Rugazia, ajali ya kwanza ilitokea katika Barabara ya
Kilwa, eneo la Msikitini, Mtoni Mtongani, saa 12.30 asubuhi jana,
ikihusisha daladala mbili aina ya Toyota DCM linalofanya safari zake
Mwenge-Mbagala na Eicher la Mbagala-Kivukoni, yaliyogongana.
Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya daladala aina ya Eicher
lililokuwa likitokea Kivukoni kuacha njia na kwenda upande wa pili wa
barabara na kuligonga daladala aina ya Toyota DCM lililokuwa likitokea
Mbagala kwenda Mwenge.
Rugazia alisema dereva wa Toyota DCM, ambaye ni mmoja wa majeruhi
alijisalimisha, lakini yule wa Eicher alikimbia baada ya ajali hiyo na
kwamba, polisi wanaendelea kumsaka.
Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa
na usukani wa Eicher kugoma kufanya kazi, hali iliyomfanya dereva wake
kushindwa kulimudu gari hilo.
Aidha, kwa mujibu wa Kaberege, jana pia walipokea hospitalini hapo
watu 11 waliojeruhiwa katika ajali iliyohusisha daladala aina Toyota
Hiace iliyogongana na Fuso.
Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kwa Sokota, wilayani
humo, majira ya saa 4 asubuhi. Hata hivyo, alisema watu hao walitibiwa
na kuruhusiwa.
MAUAJI YA PADRI MUSHI WATUHUMIWA TISA (9) WAHOJIWA
.
Jeshi la Polisi Zanzibar limeanza kuwahoji watu tisa kuhusiana na mauaji ya Padri Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoliki Zanzibar, aliyeuawa kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikana.
Padri Mushi alizikwa juzi katika makaburi ya mapadri eneo la Kitope Mkoa Kaskazini Unguja.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Yussuf Ilembo, alisema watu hao walikamatwa na kikosi kazi kilichoundwa kwa kuwahusisha maafisa wa upelelezi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
“Watu tisa tumewakamata na kuwahoji kama hatua ya kwanza kuwatafuta na kuwakamata watu waliohusika na mauaji, Tumefikia hatua kubwa ya kuwasaka watu hao,” alisema Ilembo.
Hata hivyo, alisema ni mapema kutaja majina na mitaa wanayoishi kutokana na kuhofia kuvuruga uchunguzi na kuongeza kuwa timu ya wapelelezi inaendelea na kazi yake ikiwamo kukusanya taarifa za kusaidia kuwapata wahalifu hao.
Alisema wananchi wanapaswa kulisaidia Jeshi la Polisi kutoa taarifa za siri kuhusu watu wanaowatilia shaka kuhusiana na vitendo vya hujuma dhidi ya viongozi wa dini.
Kuhusu watu watatu kudaiwa wamekamatwa huko Mombasa, Kenya, Ilembo alisema taarifa hizo hazina ukweli ingawa wanaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ndani na nje.
MAKACHERO WA NJE KUWASILI
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, alisema mpango wa kuwaleta makachero wa kimataifa umefikia hatua nzuri na wakati wowote watawasili Zanzibar.
Aboud alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kuvitaka vikosi vya ulinzi kushirikiana na kukaribisha vikosi vya nchi rafiki kufanikisha msako huo.
“Tunatafuta shina na mizizi ya uahalifu huu mahali popote ulipo, tuko tayari kumkamata mtu yeyote bila ya kujali wadhifa, cheo au jina lake,” alisema na kuongeza:
“Ndiyo maana tumeamua kukaribisha watu wenye utaalam mkubwa katika masuala ya upelelezi na lengo letui ni kukusanya ushahidi wa kutosha.”
Alisema tayari vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) vimeingia kazini kwa kushirikiana na vya Muungano na Jeshi la Polisi na kuimarisha doria maalum hasa katika maeneo nyeti ya kuingia na kutoka.
Waziri Aboud aliongeza kuwa Rais Shein ameiagiza timu ya upelelezi kumpatia taarifa ya maendeleo kila baada ya muda maalum.
ASKOFU LEBULU ATOA KAULI KALI
Akofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu, amesema, Wakristu wanao uwezo wa kulipiza kisasi dhidi ya mauaji ya viongozi wao yanayofanywa na aliowaita mashetani na mawakala wao na wangekuwa na haki ya kufanya hivyo, lakini, Kristo, anawataka wasilipize kisasi ili kumpa shetani ushindi.
“Sisi siyo wapumbavu na kwamba hatuwezi kufanya chochote…tunavutwa tu na huruma ya Mwenyezi Mungu tukae kimya, lakini hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kuvumilia hili. Katika mazingira halisi ya kibinadamu, hakuna hata mmoja ambaye atafurahia mauaji haya isipokuwa shetani na mawakala wake,” alisema.
Askofu huyo aliwataka Wakristu na waumini wa dini nyingine wenye mapenzi mema, wasitawaliwe na hasira, chuki wala mioyo ya kulipa kisasi kwa sababu Yesu Kristu amewataka wasifanye hivyo, ingawa uwezo wa kufanya hivyo wanao na haki ingekuwa upande wao.
Alisema hayo katika mahubiri yake ya Misa ya Wafu ya kumwombea marehemu Padri Mushi.
Katika misa hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu jijini hapa jana na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa dini hiyo na wa madhehebu mengine, Askofu Mkuu Lebulu, alisema: “Tusilipe kisasi, bali tushinde kwa yaliyo mema.”
“Kama Mungu yupo nasi na yupo upande wetu, hata kama kwa mabavu na bunduki, hakuna wa kututenganisha na upendo wa Kristu. Je, ni dhiki, njaa, uchi, hatari au upanga,” alihoji na kuongeza: “Lakini haya yote tunayashinda kwa Jina la Yesu na yeye anatupenda na hakuna chochote kitakachotutenga na upendo wa Kristu.”
Akizungumzia mauaji hayo, alisema wanaamini ukweli wa mambo hayo yatajulikana maana hakuna kinachotendeka kwa siri ambacho hudumu hivyo hivyo bila kujulikana.
Askofu Mkuu Lebulu, alisema Watanzania wanalia kama watoto yatima kwa kukosa baba au wazazi na akaelezea kushangazwa kwake kuhusu kauli za vitisho, matusi na kuleta hofu zilizokuwa zikisambazwa na baadhi ya watu kwa njia za CD, kanda na ujumbe wa simu, huku vyombo vya usalama vikitazama tu, halafu baadaye wanalalamika maadili yameshuka.
“Unashangaa vyombo vya usalama vinaangalia tu, zipo kanda nyingi za matusi na vitisho dhidi ya waumini wa dini nyingine…vipo wapi vyombo vya usalama kama wengine wanauawa namna hii. Mungu awaguse mioyo yao na wabadilike na kumgeukia Mungu.
“Mambo hayo watu wa usalama wamezembea, tangu awali kulikuwapo na viashiria vingi sana vya kuwapo hofu ya mauaji, lakini kwa nini hawashughulikiwi,” alihoji na kuongeza, “pengine hapa kuna siri imejificha.”
Alilaani pia mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila (45), wa Kanisa la Pentekoste la Assemblies of God, mkoani Geita, uchomaji moto wa makanisa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa Sheikh huko Zanzibar kunakofanywa na baadhi ya watu kwa malengo wanayoyajua wao wenyewe na akasema vitendo hivyo havisaidii kuleta amani ya taifa.

Saturday, February 23, 2013
WIZ KHALIFA NA AMBER ROSE WAPATA MTOTO
Amber Rose na mchumba wake Wiz Khalifa sasa ni wazazi wanaojivunia kwa
kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume.Sebastian Taylor Thomaz amezaliwa siku ya alhamis.
NA hizi ni baadhi ya picha za amber rose na Wiz Khalifa katika matukio mbalimbali akiwa mjamzito hadi mtoto wao alipozaliwa
...
..
..
....

Friday, February 22, 2013
MSANII JCB AFUNGA NDOA !! PICHA ZA HARUSI YA JCB HIZI HAPA
Msanii wa hip hop kutoka kundi la watengwa ambalo Maskani yake yapo Arusha , JCB Juzi aliuaga ukapela na Kufunga Ndoa
NA hizi ndo baadhi ya picha za harusi hiyo
...
....
...
...
HONGERA SANA JCB KWA KUVUTA JIKO

Wednesday, February 20, 2013
DIAMOND AKANUSHA KUMLOGA Q-CHIEF
.
Msanii Diamond platnumz amekana tuhuma zilizokuwa zimesambaa ,ya kuwa eti amemloga msanii mkongwe kwa game ya muziki wa bongo flava Q chillah.
hii imekuja baada ya kuwa na tuhuma zinazomuhusisha Diamond kumloga Q chief, DIAMOND amesema hausiki na kitu cha aina hiyo na hajwahi kufanya kitu kama hicho kwani hna muda huo.
Diamond amefunguka zaidi na kusema yeye anamkubali na kumuheshimu Q chief na ndio maan alipowahi kuulizwa msanii gani anaemkubali katika game ya bongo na aliyemfanya hadi akaingia kwenye muziki akamtaja Q CHIEF
amesema anashangazwa na kitendo cha Q chillah kuanza kusema Diamond amemloga,,,!!! kwani yeye hana muda wa kumloga mtu na yupo bize kufanya mambo yake ya maendeleo katika muziki na hausiki na suala hilo hata kidogo
hayo yamesemwa na DIAMOND PLATMUMZ

KUNA NINI KATI YA DIAMOND PLATNUMZ NA TANZANITE?
...
..Tanzanite
sasa hii inaleta picha ya kutoeleweka kuwa kuna nini kinaendelea kati ya diamond na msanii mwenzake tanzanite..hili linatokana na wasanii hawa kutokuwa na hali ya kuelewana kati yao kwa miaka kadhaa sasa.
Hali hii inatokana na Tanzanite kibuka na kumshtumu Diamond kuwa amemuibia wimbo wake wa ''MBAGALA'' pale alposema kuwa ni wakwake, hili lilileta mtafaruku kati yao na baada ya muda mambo yakatulia.
baadaye akachukua beat ya wimbo wa ''NITAREJEA'' wa diamond na kurekodi bila ruhusa ya diamond
Baada ya kipindi fulani tanzanite akaibuka na kusema kuwa diamond kamloga na anaumwa magonjwa ya ajbu na ameenda kwa mganga na kuambiwa kuwa diamond amemloga
akajitokeza katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini na kutangaza swala hilo na kumuomba diamond amsamehe kwa hilo.
Katika hali ya kushangaza msanii huyu tena ametoa wimbo ambao anadai ameshirikishwa na diamond,
DIAMOND amekana kuhusu kumshirikisha huyu jamaa katika huo wimbo na kuwa wimbo huo bado hajautoa na ulikuwa bado haujamalizika na huyu TANZANITE ameiba na kwenda kurekodi na kuweka sauti yake na kuuusambaza kana kwamba amefanya kolabo na diamond.
Diamond akiongea na moja ya vituo vya redio leo hii amelaani hali hii na kusema hajui huyu Tanzanite anataka nini .

Tuesday, February 19, 2013
ZANZIBAR KIMENUKA TENA!!!! KANISA LACHOMWA MOTO
Kuna
habari
za kuaminika toka kisiwani Zanzibar kuhusiana na kumwomwa moto kwa
Kanisa
alfajiri ya leo. Inasemekana Kanisa moja linalojulikana kwa jina la
SHALOOM lililopo Kusini Unguja limechomwa moto leo asubuhi na watu
wasiojulikana hali iliyosababisha baadhi ya viti vya kanisa hilo
kuungua. Inasemekana wasamaria wema waliwahi kufika eneo la tukio na
kufanikisha kuzima moto huo kabla ya kusababisha madhara zaidi. Habari
za tukio hili zimethibitishwa na Kamishna wa polisi mjini MUSA ALI MUSA
HII NDIO TATHMINI KAMILI YA MATOKEO YA FORM FOUR 2012
Ni baada ya matokeo ya taifa ya kidato cha nne mwaka huu kutangazwa hapo jana na kuzua gumzo baada ya kiwango cha ufauru kushuka kwa hali ya juu ama kwa kiasi kikubwa.
mwaka huu ufaulu wa kidato channe ni mbaya kwani wanafunzi wengi sana wamefeli.
NA HII NDO TATHMINI YA MATOKEO HAYO;
Waliofanya Mtihani - 397,136
Waliopata Daraja la 1 hadi IV - 126,847
Daraja la kwanza - 1,641
Daraja la Pili - 6,453
Daraja la Tatu - 15,426
Daraja la Nne - 103,327 SHULE ZILIZOONGOZA NI;
St. Francis Girl ya Mbeya,
Marian Boys ya Bagamoyo
Feza Boys Dar es Salaam
Marian Girls Bagamoyo,
Simini,
Kanosa na Jude
St. Mary.
Monday, February 18, 2013
PADRE AUAWA ZANZIBAR
Padri Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph- Shangani Mjini Magharibi, visiwani Zanzibar, ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi tatu kichwani huku wauaji wake wakitoroka bila kukamatwa.
Mauaji haya ni mfululizo wa hujuma dhidi ya viongozi wa dini visiwani Zanzibar na linatokea zaidi ya mwezi mmoja baada ya Padri Ambrose Mkenda, kujeruhiwa kwa kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika mwishoni mwa Desemba, mwaka jana, hadi leo waliotekeleza unyama huo hawajakamatwa.
Jana Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, aliitisha mkutano wa ghafla na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi kutoa taarifa za mauaji ya Padri Mushi, mbali ya kuthibitisha unyama huo, alisema aliuawa na watu wasiofahamika majira ya asubuhi alipokuwa anakwenda kuendesha misa katika Kanisa Katoliki la Betras lililopo eneo la Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo, alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na baadaye alifariki dunia.
Mwema alisema kutokana na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limeanza uchunguzi kuwabaini waliohusika na matukio hayo.
Aidha, alisema watu watatu wanashikiliwa kwa kuhusishwa na tukio la jana na kwamba majina yao hayawezi kutajwa hivi sasa kwa sababu za kiusalama.
MATOKEO YA FORM FOUR YAMETOKA
naibu waziri wa elimu Phillipo Mulugo
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo, aliiambia NIPASHE
katika mahojiano jana kuwa taratibu zote kwa ajili ya kutangaza matokeo
hayo zimekwisha kukamilika na sasa yatatangazwa rasmi leo.
Wiki iliyopita Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa,
akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza ajira mpya za
walimu aliahidi kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yatangazwa
mwishoni mwa wiki hiyo, lakini hata hivyo hayakutangazwa.
Dk. Kawambwa ambaye aliulizwa ni kwa nini matokeo ya mtihani huo
yanacheleweshwa kutangazwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, alisema
kimsingi hayajachelewa kwa sababu wanafunzi watakaochaguliwa kuingia
kidato cha tano wanatakiwa kuripoti mwezi Julai mwaka huu.
GHOROFA LAANGUKA DAR
....
Jengo la ghorofa nne limeporomoka eneo la Kijitonyama wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana na kusababisha kifo cha mtoto wa miaka tisa na kujeruhi mmoja.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:45 jioni baada ya nguzo za jengo hilo kutitia na kupelekea kuporomoka na hatimaye kusababisha kifo cha mtoto aliyetambulika kwa jina la Joha Jeremia.
Juhudi za kuokoa zilifanywa na kikosi cha zimamoto ambao walifanikiwa kumwokoa mfanyakazi wa nyumba hiyo aliyetambulika kwa jina la Clementina Kipanjula (19).
Mwenyekiti wa mtaa wa Mpakani B kata ya Kijitonyama Barbo Kalinga aliliambia NIPASHE kuwa ghorofa hilo lina zaidi ya miaka 20 na mmiliki wake anaitwa Charles Lukumai ambaye alishafariki miaka mingi iliyopita.
Alisema katika ghorofa hilo kulikuwa na familia yenye mama na watoto wawili pamoja na mfanyakazi wa ndani waliokuwa wanaishi.
Omary Athumani ambaye ni mlinzi wa ghorofa hilo alisema alisikia mlio wa kukatika kwa kitu lakini hakujua ni kitu gani, na ghafla akaona ghorofa linadondoka.

Sunday, February 17, 2013
WATCH NEW VIDEO ; AIKA & NAHREEL ''USINIBWAGE''
The video is good and amazing Nahreel and Aika deserve respect for this creativity
LEGO ENJOY THE VIDEO WATCH IT FROM HERE
LEGO ENJOY THE VIDEO WATCH IT FROM HERE
MAPENZI YA GOLDIE HARVEY NA PREZZO YALIKUWA NI MAIGIZO (TV SHOW) MUMEWE HALISI AJITOKEZA
Hali ya sintofahamu imezuka baada ya mtu aliyedai ndiye mume halisi wa marehemu Goldie harvey ambaye alikuwa mshiriki wa big brother africa na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamziki kutoka kenya PREZZO.
na tetesi zilizokuwepo kati ya watu hawa wawili ni kuhusu ndoa yao iliyokuwa ifanyike mwenzi huu wa pili lakini hilo halikuwezekana baada ya goldie kufariki dunia
na mtu aliyedai kuwa yeye ndo mume wa goldie amesema''Mapenzi kati ya Goldie na Prezzo yalikuwa kwa ajili ya TV SHOW''
NA HIZI NDIZO PICHA ZA HARUSI YA GOLDIE HARVEY NA MR.HARVEY NA WAKIWA PAMOJA KATIKA MAENEO TOFAUTI
.
...
...
HAPA GOLDIE AKIWA NA PREZZO

Subscribe to:
Posts (Atom)