Monday, December 31, 2012

ADAMU MCHOMVU ATOA RUKSA KUTENGENEZA VIDEO YA JONII


Mtangazaji wa show ya Double XXL na Bongo Fleva kupitia 88.5 Clouds FM radio maarufu kama Adamu Mchomvu au Baba Jonii,baada ya kutamba na ngoma yake kali inayokwenda kwa jina la Jonii,sasa leo ameamua kutoa ruksa kwa mashabiki wake kwa wale wanaotaka kutengeneza video hiyo ya Jonii.Huu ni ujumbe kutoka aliyoandika katika blog yake na kutoa ruksa hiyo"YEs,  kama  kumbukumbu zako zitakuwa  poa  basi haina shaka  utakuwa  unakumbuka  kama Jumamosi iliyopita  nilitoa  ruhusa kwa  mtu yeyote  anaona anaweza fanya  video ya  ngoma yangu matata ya 'Jonii' amabayo kitambo  kidogo ilisumbua  kwenye gemu lakini  nilikuwa sijagonga  kichupa  chake kwa  masababu kibao tu.  Round  hii nikatoa hiyo 'nike' ya watu kufanya  video na  kunitumia  nashukuru  mwitikio umekuwa  mkubwa  watu wamenigongea  4n wakisema  wameshaanza  mchakato huo na 'soon' watazidondosha  kwangu soo  kama na wewe ni mmoja wao fanya  hivyo

No comments: