Monday, February 18, 2013

MATOKEO YA FORM FOUR YAMETOKA

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/10/Philipo-Mulugo.jpg     naibu waziri wa elimu Phillipo Mulugo

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
 Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Philipo Mulugo, aliiambia NIPASHE katika mahojiano jana kuwa taratibu zote kwa ajili ya kutangaza matokeo hayo zimekwisha kukamilika na sasa yatatangazwa rasmi leo. 
 Wiki iliyopita Waziri wa wizara hiyo, Dk. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza ajira mpya za walimu aliahidi kuwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yatangazwa mwishoni mwa wiki hiyo, lakini hata hivyo hayakutangazwa.
 
Dk. Kawambwa ambaye aliulizwa ni kwa nini matokeo ya mtihani huo yanacheleweshwa kutangazwa ukilinganisha na miaka ya nyuma, alisema kimsingi hayajachelewa kwa sababu wanafunzi watakaochaguliwa kuingia kidato cha tano wanatakiwa kuripoti mwezi Julai mwaka huu.

No comments: